Immanuel Kant - Wikipedia, kamusi elezo huru Immanuel Kant Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru Jump to navigation Jump to search Immanuel Kant Taswira ya Immanuel Kant Alizaliwa 22 Aprili 1704 Alikufa 12 Februari 1804 Nchi Prussia (Ujerumani) Kazi yake profesa wa chuo kikuu mwanafalsafa Immanuel Kant alikuwa mwanafalsafa Mjerumani kutoka milki ya Prussia. Anahesabiwa kati ya wanafalsafa muhimu zaidi wa zama za mwangaza. Yaliyomo 1 Maisha 2 Falsafa 3 Mwanafalsafa wa mwangaza 4 Ngazi ya urazini 5 Ngazi ya Uhakiki 6 Maswali 4 ya Kant 7 Uhakiki wa akili tupu 8 Uhakiki wa akili tendaji 9 Viungo vya Nje Maisha[hariri | hariri chanzo] Kant alizaliwa mjini Königsberg (sasa: Kaliningrad) kama mtoto wa fundi. Mamake alimsomesha kweye shule ya sekondari akaendelea kusoma tholojia, falsafa, sayansi, fizikia na hisabati. Tasnifu (thesis) yake ya kwanza haikupokelewa na profesa wake mwaka 1746 hivyo alifanya kazi ya mwalimu kwenye nyumba ya matajiri na makabaila mbalimbali kwenye mazingira ya Königsberg. 1754 alirudi kwenye chuo kikuu akamaliza masomo yake. Tangu 1755 alikuwa mwalimu na tangu 1870 profesa kamili kwenye chuo kikuu cha Königsberg. Hakuoa aliishi na mtumishi wa nyumbani tu hadi kifo chake mwaka 1804 kwa umri wa miaka 80. Kaburi lake ni kando la kanisa kuu la Königsberg limetunza hata siki hizi baada ya kufukuzwa kwa Wajerumani na kuwa sehemu ya Urusi. Falsafa[hariri | hariri chanzo] Mwanafalsafa wa mwangaza[hariri | hariri chanzo] Kwa Kant kazi ya akili inaanza kwa kufikiri mwenyewe. Alisema "Sapere aude!" na hii inamaanisha : "Usiogope kutafakari mwenyewe". Aliona ni muhimu ya kwamba kila mtu anatumia akili yake mwenyewe badala ya kutegemea mawazo ya watu wengine. Mawazo na mafundisho yote yanapaswa kupitia kwenye uhakiki wa akili. Kwa njia hii alitafsiri mwelekeo wa zama za mwangaza na wengi wanamwona kuwa alikamilisha jitihada za mwangaza. Kant aliandika: "Mwangaza inamaanisha kuondoka kwa binadamu kutoka uchanga wake uliosababisha mwenyewe. Uchanga unamaanisha kutotumia akili bila mwongozo wa mwingine. Uchanga huu husababishwa na mtu mwenyewe si kwa sababu ya uhaba wa akili lakini kwa sababu ya uhaba wa nia na hofu ya kutumia akili bila mwongozo wa mwingine." Ngazi ya urazini[hariri | hariri chanzo] Katika kutafakari kwake Kant alipita njia. Mara nyingi hii inagawiwa katika vipindi viwili: labla ya "uhakiki" na baada ya "uhakiki"". Tangu kutunga kitabu chake cha "Uhakiki wa akili tupu" alifundisha tofauti kuliko awali. Katika kipindi cha kwanza hadi 1860 alifuata mtindo wa walimu wake uliotiwa urazini (rationalism). Alirudia jinsi alivyofundishwa na wanafalsafa kama Leibnitz ya kwamba akili inaweza kutambua kila kitu. Ngazi ya Uhakiki[hariri | hariri chanzo] Katika tasnifu yake alianza kusogea mbali na urazini unaofundisha ya kwamba akili inaweza kutambua ulimwengu na hali halisi ya vitu vyote. Kant alisisitiza ya kwamba si akili peke yake lakini pia maarifa na ufahamu. Kuona ni muhimu kama kutafakari. Kazi ya falsafa aliona katika kufikiria uhusiano wa yale yanayopatikana akilini kama dhana na yale yanayonekana hali halisi katika mazingira ya mtu. Msingi huu ulikuwa mpya ukalazimisha kutafakari upya maswali mengi katika falsafa hasa metafizikia. Baada ya kupokea wito la kuwa profesa Kant alikuwa na kipindi nyamavu cha miaka 10 maana yake alifundisha wanafunzi wake lakini hakutoa kitabu kipya akitafakari yale yanayofuata kutokana na msingi wake mpya. Alihitaji kuujibu swali jinsi gani binadamu anapata ujuzi wake na jinsi ganz akili inaweza kuishughulikia. Maswali 4 ya Kant[hariri | hariri chanzo] Kant alijiuliza maswali manne: 1. Ninaweza kujua nini? 2. Ninatakiwa kufanya nini? 3. Ninweza kutumaini nini? 4. Binadamu ni nini ? Uhakiki wa akili tupu[hariri | hariri chanzo] Mwaka 1871 alitoa kitabu cha "uhakiki wa akili tupu". Humo aliuliza swali je akili inaweza kujua nini bila maarifa. Anaangalia ujuzi wa "a priori" (Kilatini: kutoka chanzo). KUna mambo ambayo tunajua bila maarifa na ujuzi huu ni msingi wa kupata maarifa. Tunajua kuwepo kwa wakati na mahali bila kuiona - na kw aujuzi huu ndani yetu hatuwezi kuelewa wakati fulani au mahali fulani. Hapa anaita hisabati aina ya "sayansi a priori" kwa sababu dhana zote za hisabati ziko bila maarifa yoyote. Halafu antazama mipaka ya akili. Akili inataka kuendelea lakini inagonga mipaka. Maswali kama: Je kuna roho ndani ya mtu isiyokufa? Kuna Mungu? Dunia haina mipaka? yanahusu mambo ambayo akili haiwezi kujibu kwa uhakika. Hakuna uthebitisho kwa namna ya uthebitisho wa kisayansi. Uhakiki wa akili tendaji[hariri | hariri chanzo] "Uhakiki wa akili tendaji" ni kitabu cha pili kinachoendeleza kile cha kwanza. Akili tendaji ni matumizi ya akili kwa maadili ya kutenda yale ambayo ni mema na sahihi. Hapa anafundisha "amri halisi": "Katika matendo yako fuata shabaha hizi tu zinazofaa kuwa msingi wa sheria kwa watu wote." Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo] Wikimedia Commons ina media kuhusu: Immanuel Kant Works by Immanuel Kant in audio format from LibriVox Immanuel.Kant,Critique of Pure Reason (1787 (english) Internet Encyclopaedia of Philosophy The Internet Encyclopaedia of Philosophy has several topics about Kant Immanuel Kant in Italia A Website on the presence and diffusion of the philosophy of Immanuel Kant in Italy Stephen Palmquist's Glossary of Kantian Terminology Kant's Categories as grammatical reifications Kant's Ethical Theory Kantian ethics explained, applied and evaluated Kant & Ethics Extensive links and discussions from Lawrence Hinman at University of San Diego Notes on Deontology A conveniently brief survey of Kant's deontology Kant's Ethics in Italy today Contemporary Italian writings about Kant's Ethics North American Kant Society (NAKS) Kant on the Web on Stephen Palmquist's website Kant Links Kant's Epistemology and Metaphysics according to the Friesian school Kant and the project of enlightenment German Idealist Foundations of Durkheim's Sociology and Teleology of Knowledge Several Kant's works in clickable pdf Routledge Encyclopedia of Philosophy (14 sections on Kant) International Kant Interview - 2004 Readable versions of Prolegomena, Groundwork for the Metaphysic of Morals, and Critique of Pure Reason All works of Kant (German) Kant's moral philosophy and the question of pre-emptive war, Revue Sens Public Kant in the Classroom (background information for Kant's lectures) Immanuel Kant's works: text, concordances and frequency list Kant On Race and Development Michel Foucault's Dissertation on Kant's Anthropology Kant on property Part one of 'The Critique of Aesthetic Judgment' The Stanford Encyclopedia of Philosophy has several entries on Kant: Kant's Philosophy of Science Kant's Critique of Metaphysics Kant's View of the Mind and Consciousness of Self Kant's Aesthetics and Teleology Kant's Philosophy of Religion Kant's Philosophical Development Kant's Moral Philosophy Kant and Leibniz Kant's Theory of Judgment Kant's Fourth Critique Italian writings Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Immanuel_Kant&oldid=948266" Jamii: Waliozaliwa 1704 Waliofariki 1804 Watu wa Prussia Wanafalsafa wa Ujerumani Urambazaji Vifaa binafsi Hujaingia Majadiliano ya IP hii Michango Unda akaunti Ingia Maeneo ya wiki Makala Majadiliano Vibadala Mitazamo Soma Hariri Hariri chanzo Fungua historia More Tafuta Urambazaji Mwanzo Jumuia Matukio ya hivi karibuni Mabadiliko ya karibuni Ukurasa wa bahati Msaada Michango Vifaa Viungo viungavyo ukurasa huu Mabadiliko husika Pakia faili Kurasa maalum Kiungo cha daima Maelezo ya ukurasa Taja ukurasa huu Wikidata item Chapa/peleka nje Tunga kitabu Pakua kama PDF Ukurasa wa kuchapika Miradi mingine Wikimedia Commons Lugha zingine Afrikaans Alemannisch አማርኛ Aragonés العربية الدارجة مصرى Asturianu Aymar aru Azərbaycanca تۆرکجه Башҡортса Žemaitėška Bikol Central Беларуская Беларуская (тарашкевіца)‎ Български भोजपुरी বাংলা Brezhoneg Bosanski Буряад Català Chavacano de Zamboanga Нохчийн Cebuano کوردی Čeština Чӑвашла Cymraeg Dansk Deutsch Zazaki Ελληνικά Emiliàn e rumagnòl English Esperanto Español Eesti Euskara Estremeñu فارسی Suomi Võro Føroyskt Français Arpetan Nordfriisk Frysk Gaeilge 贛語 Kriyòl gwiyannen Gàidhlig Galego ગુજરાતી עברית हिन्दी Fiji Hindi Hrvatski Magyar Հայերեն Interlingua Bahasa Indonesia Interlingue Ilokano Ido Íslenska Italiano 日本語 Patois Jawa ქართული Qaraqalpaqsha Taqbaylit Kabɩyɛ Қазақша ಕನ್ನಡ 한국어 Kurdî Кыргызча Latina Lëtzebuergesch Лезги Lingua Franca Nova Limburgs Ligure Ladin Lumbaart لۊری شومالی Lietuvių Latviešu मैथिली Malagasy Македонски മലയാളം Монгол मराठी Кырык мары Bahasa Melayu Malti Mirandés မြန်မာဘာသာ Эрзянь Nāhuatl Plattdüütsch नेपाली नेपाल भाषा Nederlands Norsk nynorsk Norsk bokmål Occitan Livvinkarjala ਪੰਜਾਬੀ Polski Piemontèis پنجابی پښتو Português Runa Simi Rumantsch Română Русский Русиньскый Kinyarwanda संस्कृतम् Саха тыла Sardu Sicilianu Scots Srpskohrvatski / српскохрватски Simple English Slovenčina Slovenščina Shqip Српски / srpski Sunda Svenska தமிழ் తెలుగు Тоҷикӣ ไทย Tagalog Tok Pisin Türkçe Татарча/tatarça Українська اردو Oʻzbekcha/ўзбекча Vepsän kel’ Tiếng Việt West-Vlams Volapük Winaray 吴语 მარგალური ייִדיש Yorùbá Zeêuws 中文 文言 Bân-lâm-gú 粵語 Hariri viungo Ukurasa huu umebadilishwa kwa mara ya mwisho tarehe 22 Aprili 2015, saa 21:37. Maandishi yanapatikana chini ya leseni ya Creative Commons Attribution-ShareAlike License; matakwa mengine yanaweza kutakiwa. Tazama maelezo zaidi ya Matakwa ya Utumiaji. Sera ya faragha Kuhusu Wikipedia Kanusho Mtazamo wa rununu Developers Statistics Cookie statement